Jumatano, 6 Mei 2020

             

MITIHANI NA MAJARIBIO KWA SHULE ZA MSINGI PITIA LINK ZIFUATAZO;
         ENGLISH DARASA LA TANO BOFYA HAPA CHINI.
https://1drv.ms/w/s!AphBaL_mADgKgV5TfHpQGRuGIdRD

             HISABATI DARASA LA SITA BOFYA HAPA CHINI;
                https://1drv.ms/w/s!AphBaL_mADgKgV9iRPpBwCOnyvLH

Jumamosi, 14 Aprili 2018

Jumanne, 20 Machi 2018

UFALME WA MBINGUNI

    UFALME WA MBINGUNI

              Shabaha kuu ya mafundisho ya YESU  ni kuleta Ufalme wa Mbinguni katika Taifa lake teule na kisha katika Ulimwengu mzima kwa njia ya hili Taifa kama ulivyokuwa utawala wa Kiisraeli katika Agano la kale.
                 Watakatifu ndio raia wa ufalme huo,  na Mungu ndiye Mfalme wao kweli. Hao ni raia wake kwasababu utawala wake wataukubali katika kumjua na kumpenda.
                      Ufalme huo ulitetereka kwa dhambi ya Adamu.  Na sasa imempasa Mungu Mwenyezi kuutengeneza upya katika Masiya wake.
      Danieli2:28a "Lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri,"  Ndiyo sababu Yesu anatangaza sasa kama alivyofanya Yohana Mbatizaji, ya kuwa Mungu amekwisha jitia kati yao.  Mt 3:2 "wakamvizia ili kuona kama atamponya siku ya Sabato,  wapate kumshitaki"~

Jumamosi, 3 Machi 2018

TUTAFAKARI MAANA YA UBATIZO.

                      UBATIZO
Katika nyakati hizi za kuutafuta na kuukulia wokovukumekuwa na kutoelewana miongoni mwa waamini/wafuasi wa Kristo.
Tofauti zao zimetokana na taratibu zinazotumika katika kutimiza agizo la Mungu

       Mathayo 28: 19-20
"Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzimkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana,na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyiNa tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zotehata ukamilifu wa dahari. "

        Maana ya ubatizo.
Ubatizo wa YOHANE MBATIZAJI, Katika Kiyunani maana yake kutosa majini
      Ibada ya kutosa mwili majini ni mfano wa utakaso au wa kujitengeneza upyaIbada kama hiyo ilijulikana na kutendeka katika dini za kale za kipagani na dini za Kiyahudi pia(mfano ubatizo wa Waongofu>matendo 2:10). Ingawa YOHANE atumia ibada kama hiyoubatizo wake ni tofauti sana na ubatizo wao kwa sababu zifuatazo: -
   Ubatizo wao uliwatakasa watu nje nje tu,
    Tena ,ulirudiwarudiwa,
     Halafu, haukuwa alama ya nyakati za Masiya.
UBATIZO WA YOHANE wataka kuwatakasa watu mioyoni mwao "mathayo 3: 2,6 ,8,11(Tubuni kwa maana ufalme wa Mbinguni umekaribia..... Naye akawabatiza katika mto Yordanihuku wakiziungama dhambi zao...Basi zaeni matunda yapasayo toba........kweli mimi nawabatiza kwa maji kwaajili ya toba ; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimiwala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto usiozimika. Pia rejea >>Luka 3: 10-14 "Makutano wakamuulizatufanye nini basiAkawajibu akiwaambia, " mwenye kanzu mbili na ampe asiye na kanzu.; na mwenye vyakula na afanye vivyo hivyoWatoza ushuru nao wakaja kubatizwawakamuuliza "Mwalimu tufanye nini sisi? Akawaambia msitoze kitu zaidi kuliko mlivyoamriwa;,  Askari nao wakamuulizawakisema " Sisi nasi tufanye nini? Akawaambiamsidhulumu mtuwala msishitaki kwa uongotena mtoshewe na mshahara wenu.
       Ubatizo huu hutumika mara moja tu bila kurudiwana hivyo ni alama ya kumwingiza mtu katika maisha mengine. Tena ni utangulizi unaotumainisha ujio wa nyakati za MasiyaUnawatumainisha waamini wake kwamba Masiya yu karibunao wajiunda shirika kabla ya kuwasili Masiya mwenyewe.
      Ubatizo huo wa Yohane ulikuwa na nguvu kwelinguvu yake ilitegemea hukumu ya Mungu iliyofika baadaye katika NAFSI ya MASIYA mwenyewe. Huyo ndiye atakaye watakaa kwa moto watu waliojiweka tayari. Yeye peke yake atawabatiza katika ROHO MTAKATIFUUbatizo wa Yohane waliendelea kuutumia Wafuasi wa KRISTO "Yohana 4: 1-2 Kwahiyo Bwana alipofahamu ya kuwa Mafarisayo wamesikia ya kwamba Yesu anafanya wanafunzi wengi kuliko Yohanena kuwabatiza 2.lakini Yesu mwenyewe hakubatizabali wanafunzi wake."
    Ubatizo huo utatumika mpaka utakapotanguliwa na Yesu kwa kuwekwa namna mpya ya ubatizo. (Matendo 1: 5 "ya kwamba Yohane alibatiza kwa majibali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache." Rumi 6:4 "Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yakekusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba,  vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima" )
  YESU ANABATIZWA, Ingawa Yesu hakuwa na dhambi "Yohana 8: 46 Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli mbona hanni sadiki? "
  YESU alikubali kubatizwa na YOHANE kwani hiyo ndiyo hatua aliyotaka MUNGU "Luka 7: 29-30 Na watu wote na watoza ushuru waliposikia hayowalikiri haki ya Mungukwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohane. LakiniMafarisayo na Wanasheria  walilipinga shauri la Mungu juu yaokwakuwa hawakubatizwa naye. "
  Kubatizwa kwa Yesu ilikuwa ni matayarisho ya mwisho kwaajili ya nyakati za Kimasiya. Kwa kitendo hicho Yesu alitaka kuridhisha haki ya Mungu awezayo kuidai ili sisi tupate wokovu "mathayo 3: 15 Yesu akajibu akamwambia "kubali hivi sasa, kwakuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akakubali. " 
        Katika kitendo hicho cha ubatizoMwinjili Mathayo afikiri pia haki mpya  ya Yesu ambayo kwayo ataitimiliza na kuikamilisha haki ya Agano la Kale "Mathayo 5: 17-20 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua Torati au Manabii; lasikuja kutangua bali kutimiliza. 18.kwa maana Amin,  nawaambiampaka mbingu na nchi zitakapoondolewa, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka hata yote yatimie.  19.Basi mtu yeyote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni.  Bali mtu atakayezitenda na kuzifundishahuyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.  20.Maana nawaambia haki yenu isipozidi hiyo haki ya Waandishi na Mafarisayohamtaingia kamwe katika Ufalme wa Mbinguni.
      UBATIZO WA KIKRISTO. Huu ni ubatizo katika Roho Mtakatifu kama ilivyotangazwa na Yohane Mbatizaji(mt 3: 11 ) . Pia Yesu anaahidi ubatizo huo utaanza na kumiminwa kwa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste "matendo 2: 1-4 Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwapo wote mahali pamoja. Kukaja ghafla toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasiukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana,  kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine,  kama Roho alivyowajalia kutamka. "
    Halafu Mitume wataendelea kutoa ubatizo na maji "matendo2: 41 ~Nao waliolipokea Neno lake Wakabatizwana siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.  8: 12,38~Lakini walipomwamini Filipoakizihubiri habari njema za ufalme wa Munguna jina lake Yesu Kristo wakabatizwa wanaume na wanawake,  38~Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majiniFilipo na yule Towashi; naye akambatizaRejea pia matendo 9: 18, 10: 48, 16: 15,33
      Kadiri ya maagizo ya KRISTO(MT 28: 19) ni kama unyago wa kumwingiza mtu katika Ufalme wa Masiyalakini watatoa ubatizo huo katika Jina la Yesu "mdo 2: 38~Petro akawaambia " Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenunanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. "
       Tena ubatizo huo utatolewa kwa yule mwenye kusadiki  katika matendo ya wokovu ya Yesu, "Rumi6: 4~Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yakekusudi la Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.
     Ubatizo na Imani Huandamana pamoja, "Galatia 3: 26-27~Kwakuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya Imani katika Kristo YesuMaana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. "Efeso 4: 5~Bwana mmoja, Imani mojaUbatizo mmoja." "Ebrania 10: 22~na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imanihali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbayatume ishwa miili kwa maji safi. "
          Mapato ya ubatizo huu ni yale yale "Galatia 2: 16-20~hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria bali kwa imani ya Kristo Yesu, sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakaye hesabiwa hakiLakini ikiwa Sisi wenyewe kwa kutafuta kuhesabiwa haki katika Kristo,  tulionekana kuwa wenye dhambije, Kristo amekuwa mtumishi wa dhambiHashaMaana nikiyajenga tena yale niliyoyabomoanaonyesha ya kuwa mimi mwenyewe ni mkosajiMaana mimi kwa njia ya sheria naliifia sheria ili nimwishie Mungu. Nimesulibiwa pamoja na Kristo,  lakini ni haiwala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yanguna uhai nilio nao sasa katika mwilininao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda akajitoa nafsi yake kwaajili yangu. Rejea pia Rumi 6: 3-9
       Ubatizo wa Kikristo una nguvu ya kuondolea dhambi na kumpa mtu Roho Mtakatifu (mdo 2:38)
Watu wa zamani hubatizwa kwa kutosha majinina maana ya neno ubatizo kwa Wagiriki ni kutoka majiniTendo hili la kutosha na kutoka majini latumika na Paulo kama mfano "Rumi 6: 3-7~Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesutulibatizwa katika mauti yakeBasi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama tulivyounganika naye katika mfano wa mauti yakekadhalika tutaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake. Tukijua neno hili ya kuwa utu wetu wa kale Ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tuitumikie dhambi tena. Kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi.
      Kutoswa majini maana yake mkosefu azikwa pamoja na Kristo "Kolosai 2: 12~mkazikwa pamoja naye katika ubatizona katika huo mkafufuliwa pamoja nayekwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu"
        Kutoka majini maana yake mkosefu afufuka na Kristo "Rumi 8: 11~Lakini ikiwa Roho wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufakwa Roho wake anayekaa ndani yenu" ili awe kiumbe kipya au mtu mpya "2kor5: 7, Efeso 2: 15" au viungo vya mwili mmoja vihuishwavyo na Roho mmoja "1kor 12: 13"
         Ufufuko huo utakuja kukamilika mwisho wa dunia "1kor15: 12~Basi,  ikiwa Kristo anahubiriwa yakwamba amefufuka katika wafumbona baadhi yenu husema kwamba hakuna ufufuo wa wafu?
         MAANA YA UBATIZO KADIRI YA
                            BIBLIA
Ubatizo kadiri ya Biblia  unaelezwa kwa habari nyingine zaidi ya huko kufa na kufufuka katika Kristo.
         Maana za ubatizo Kibiblia ni: -
  Kumtakasa mtu (Efeso 5: 26>ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika NenoEbrania 10: 22>Na tukaribie wenye moyo wa kweli kwa utimilifu wa imanihali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbayatumeshaona miili kwa maji safi)
     Pengine ni kuzaliwa kupya(Yohana 3: 5>Yesu akajibu, "Amin, Amin, nakuambia; Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Rohohawezi kuuingia ufalme wa Mungu,  Tito 3: 5>si kwasababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi, bali kwa rehema yake, kwa kuoshwakwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu. )
      Pengine ni kuangazwa kupya(Ebrania 6: 4>Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru na kulionja kipawa cha Mbinguni na kufanywa washiriki wa Roho Mtakatifu, 10: 32>Lakini zikumbukeni siku za kwanza ambazo mlipokwisha kutiwa nuru, mlistahimili mashindano makubwa ya maumivu)
      Kadiri ya 1Petro 3: 21, safina ya Nuhu ni mfano wa ubatizo. (Mfano wa mambo hayo ni ubatizo unaowaokoa ninyi pia siku hizisiyo kuwekea mbali uchafu wa mwilibali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.
       Ubatizo mfano wa mateso ya Kristo(Marko 10: 38>Yesu akawaambia, "hamjui mnaloomba. Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi,  au kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi?,  Marko 14: 36>Akasema, " Aba,  Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; walakini si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe)

     
    NB:       sijaona mahali katika Biblia ubatizo ulifanyika mahali pengine tofauti na mto Yordani.
                    Kisha nikajiuliza kwanini waamini wa leo hatuendi kubatizwa mto Yordani?

JIBU NILILOPATA: ni taratibu zilizowekwa na washirika ili kufanikisha kwa urahisi na kwa watu wote agizo la BWANA YESU.
               Nikajiuliza tena wamewezaje kuweka taratibu hizowamepata wapi kibali?

JIBU NILILOLIPATAni mathayo 18: 19-20>>Tena nawaambia ya kwambawawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliombawatafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwakuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langunami nipo katikati yao.

          Hapo nikaishiwa maswali.

                            Je,
                 wewe una maswali?





                 BARIKIWA SANA.

NI MIMI,
            MFUASI NA MWANAFUNZI
                    WA YESU KRISTO
    
                 BADIANI Z. KINWIKO.
               
             



Ijumaa, 2 Machi 2018

ADUI MKUBWA WA MTU NI MWILI WAKE.

                  ADUI WA MTU
                             NI
                   MWILI WAKE:

Warumi 8:6
Kwakuwa nia ya mwili ni mauti, Bali karama ya Roho ni uzima, Na amani.

Mauti  ni kifo,  
    Sijaona mtu anayependa mauti popote,  na ndio maana tunasema adui mkubwa
ni mwili wako mwenyewe kwani tangu zamani shauku ya mwili ni mauti. 

Mwanadamu  yupo katika sehemu kuu tatu za maamuzi,  ambazo ni: -
         i.   Mwili
        ii.     Nafsi
        iii.    Roho. 
Nafsi ndio hutekeleza maagizo yanayotolewa na Mwili au Roho,  kutegemeana na
kile kinachotawala mwanadamu huyo kwa wakati huo,  au kwa lugha rahisi chenye 
nguvu kuliko kingine. 
Mwili na Roho, huwa vina shindana kila siku,  kila wakati kuhusu kupeleka maamuzi
kwenye nafsi (Galatia 5:17)
             "kwasababu Mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na
 mwili,  kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka".

Kwa lugha nyepesi ni kusema kwamba ndani ya mwanadamu kuna falme mbili zinazopigania madaraka katika kuamrisha nafsi ifanye jambo. 
Ndio maana Biblia inasema " hata hamwezi kufanya mnayotaka" na wakati 
mwingine Paulo alikiri kupatwa na jambo hilo kwakusema "lile ninalotaka nilitende
silitendi,  na lile nisilotaka kutenda ndilo nalitenda" 
  Kumbe tatizo lipo kwa yule tuliyempa nafasi ya kuongoza Maisha yetu,  na ndiye anaye
tupelekea kufanya mambo mbalimbali. 

       Mtu anapokuwa anaongozwa au yuko chini ya utawala wa mwili hufanya sawasawa na mapenzi ya mwili, au vile dunia inavyotaka.  Na ifahamike kuwa mwili hautosheki /hauridhiki  kila siku vitu vinavyovutia hutokezea na kuvutia mwili au kuutamanisha mwili na hivyo mtu huyu huweka nia na nguvu kubwa kuvipata vitu hivyo hata kama vina anguko kubwa. 

Mtu aliye chini ya utawala wa mwili Biblia inaweka wazi matendo yake anayofanya katika Galatia 5: 19-21, 
  "Basi matendo ya mwili ni dhahiri,  ndiyo haya: -
1.uasherati,
2.Uchafu
3.Ufisadi,
4.Ibada ya sanamu,
5.uchawi,
6.uadui,
7.ugomvi,
8.wivu,
9.hasira,
10.fitina,
11.faraka,
12.uzushi,
13.husuda,
14.ulevi,
15.ulafi na mambo yanayofanana na
        hayo.

Kila anayefanya matendo hayo na mengine yanayofanana na hayo ni dhahiri kwamba anaongozwa na mwili  na yupo kinyume na nia ya Mungu.
         Warumi 8: 8 "wale wafuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu"
  Kwa maana nyingine hawawezi kutembea katika imani,  kwa maana ili mtu ampendeze Mungu ni lazima atembee katika imani.
           Ebrania 9: 6" Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungukwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yukona kwamba huwapa thawabu wale wamfuatao"

Ili tuweze kumpendeza Mungu ni lazima kila mtu autiishe mwili wake na kuipa Roho nguvu,  ndio maana tunashauriwa tuwe na tabia ya kufanya maombi ya mfungo mara kwa mara,  kwani lengo kubwa la kufunga huwa ni kuutiisha mwili na kuruhusu Roho itoe amri katika Nafsi maana nia ya ROHO ni UZIMA na AMANI.
         Galatia 5: 16 "BASI NASEMA:  ENENDENI KWA ROHO,  WALA HAMTAZITIMIZA KAMWE TAMAA ZA MWILI"

         
          BARIKIWA SANA!!

         NI MIMI,
                    BADIANI Z. KINWIKO
               MFUASI NA MWANAFUNZI
                                   WA
                          YESU KRISTO.
              

           

Jumanne, 4 Aprili 2017

AMRI KUMI ZA MUNGU

TUJIFUNZE AMRI ZA MUNGU /Kutoka 20:1-20
1. Mimi ni Bwana Mungu wako,  usiwe na miungu mingine ila mimi. 
Tunapaswa kumwogopa Mungu kwa kutotenda makosa, dhambi,  au uovu
katika maisha yetu tuwapo duniani. 
Tena tunapaswa kumpenda Mungu wetu tukijua kuwa alitukomboa kutoka
utumwani kwenye mateso mengi. 
Kadhalika,  tuweze kumtegemea yeye kwa kila hitaji. 
NB. Vitu vyote chini ya jua vimeumbwa na Mungu,  kwahiyo hatupaswi
         kuvipatia sifa anazostahili kupewa Mungu. 
        
       Swali:
1. Umewahipatwa na tatizo lolote gumu kiasi cha kukufanya ukose uamuzi? 
2. Umewahi kuwa na furaha kubwa kiasi cha kujiona huhitaji msaada? 
NOTE: ikiwa ulikutana na mambo hayo mawili,  hatua ya kwanza ulifanya nini? 

Sikia mpendwa "ukiwa na shida au tatizo tunapaswa kumwangalia Mungu
kwanza,  usiweke utatuzi kupitia fedha au ndugu au kitu chochote kisha 
ndo umwite Mungu.  Anza na Mungu ndipo mengine yafuate. 

Unaitumikia mali, duka, simu au watu?
Unamtumikia Mungu? 
        Kusoma Neno ndani ya biblia
       . kuhubiri Neno la Mungu
       . kuwasaidia wenye shida
       . kuwa kielelezo kwa mwenendo mwema,  tabia njema,  na matendo meme. 
        . kufunga kwaajili ya kazi ya Mungu
         . kuishi maisha ya sala ukiombea huduma ya Neno la Mungu
         . kuwatembelea wagonjwa na kuwafariji. nk. 
Huku ndiko kumtumikia Mungu. 



Soma zaidi:
 Mathayo 4:10, 6:24, 10:28, 22:37, 
 1yohana 2:15-17,  4:19




UBARIKIWE NA BWANA

NI MIMI
MTUMISHI NA MFUASI WA
YESU KRISTO, 

BADIANI KINWIKO.