Ijumaa, 19 Mei 2017
Jumanne, 4 Aprili 2017
AMRI KUMI ZA MUNGU
TUJIFUNZE AMRI ZA MUNGU /Kutoka 20:1-20
1. Mimi ni Bwana Mungu wako, usiwe na miungu mingine ila mimi.
Tunapaswa kumwogopa Mungu kwa kutotenda makosa, dhambi, au uovu
katika maisha yetu tuwapo duniani.
Tena tunapaswa kumpenda Mungu wetu tukijua kuwa alitukomboa kutoka
utumwani kwenye mateso mengi.
Kadhalika, tuweze kumtegemea yeye kwa kila hitaji.
NB. Vitu vyote chini ya jua vimeumbwa na Mungu, kwahiyo hatupaswi
kuvipatia sifa anazostahili kupewa Mungu.
Swali:
1. Umewahipatwa na tatizo lolote gumu kiasi cha kukufanya ukose uamuzi?
2. Umewahi kuwa na furaha kubwa kiasi cha kujiona huhitaji msaada?
NOTE: ikiwa ulikutana na mambo hayo mawili, hatua ya kwanza ulifanya nini?
Sikia mpendwa "ukiwa na shida au tatizo tunapaswa kumwangalia Mungu
kwanza, usiweke utatuzi kupitia fedha au ndugu au kitu chochote kisha
ndo umwite Mungu. Anza na Mungu ndipo mengine yafuate.
Unaitumikia mali, duka, simu au watu?
Unamtumikia Mungu?
Kusoma Neno ndani ya biblia
. kuhubiri Neno la Mungu
. kuwasaidia wenye shida
. kuwa kielelezo kwa mwenendo mwema, tabia njema, na matendo meme.
. kufunga kwaajili ya kazi ya Mungu
. kuishi maisha ya sala ukiombea huduma ya Neno la Mungu
. kuwatembelea wagonjwa na kuwafariji. nk.
Huku ndiko kumtumikia Mungu.
Soma zaidi:
Mathayo 4:10, 6:24, 10:28, 22:37,
1yohana 2:15-17, 4:19
UBARIKIWE NA BWANA
NI MIMI
MTUMISHI NA MFUASI WA
YESU KRISTO,
BADIANI KINWIKO.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)

