Jumamosi, 3 Machi 2018

TUTAFAKARI MAANA YA UBATIZO.

                      UBATIZO
Katika nyakati hizi za kuutafuta na kuukulia wokovu,  kumekuwa na kutoelewana miongoni mwa waamini/wafuasi wa Kristo.
Tofauti zao zimetokana na taratibu zinazotumika katika kutimiza agizo la Mungu, 

       Mathayo 28: 19-20
"Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi,  mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana,na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi.  Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote,  hata ukamilifu wa dahari. "

        Maana ya ubatizo.
Ubatizo wa YOHANE MBATIZAJI, Katika Kiyunani maana yake kutosa majini. 
      Ibada ya kutosa mwili majini ni mfano wa utakaso au wa kujitengeneza upya.  Ibada kama hiyo ilijulikana na kutendeka katika dini za kale za kipagani na dini za Kiyahudi pia(mfano ubatizo wa Waongofu>matendo 2:10). Ingawa YOHANE atumia ibada kama hiyo,  ubatizo wake ni tofauti sana na ubatizo wao kwa sababu zifuatazo: -
   Ubatizo wao uliwatakasa watu nje nje tu,
    Tena ,ulirudiwarudiwa,
     Halafu, haukuwa alama ya nyakati za Masiya.
UBATIZO WA YOHANE wataka kuwatakasa watu mioyoni mwao "mathayo 3: 2,6 ,8,11(Tubuni kwa maana ufalme wa Mbinguni umekaribia..... Naye akawabatiza katika mto Yordani,  huku wakiziungama dhambi zao...Basi zaeni matunda yapasayo toba........kweli mimi nawabatiza kwa maji kwaajili ya toba ; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi,  wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto usiozimika. Pia rejea >>Luka 3: 10-14 "Makutano wakamuuliza,  tufanye nini basi?  Akawajibu akiwaambia, " mwenye kanzu mbili na ampe asiye na kanzu.; na mwenye vyakula na afanye vivyo hivyo,  Watoza ushuru nao wakaja kubatizwa,  wakamuuliza "Mwalimu tufanye nini sisi? Akawaambia msitoze kitu zaidi kuliko mlivyoamriwa;,  Askari nao wakamuuliza,  wakisema " Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia,  msidhulumu mtu,  wala msishitaki kwa uongo,  tena mtoshewe na mshahara wenu.
       Ubatizo huu hutumika mara moja tu bila kurudiwa,  na hivyo ni alama ya kumwingiza mtu katika maisha mengine. Tena ni utangulizi unaotumainisha ujio wa nyakati za Masiya.  Unawatumainisha waamini wake kwamba Masiya yu karibu,  nao wajiunda shirika kabla ya kuwasili Masiya mwenyewe.
      Ubatizo huo wa Yohane ulikuwa na nguvu kweli,  nguvu yake ilitegemea hukumu ya Mungu iliyofika baadaye katika NAFSI ya MASIYA mwenyewe. Huyo ndiye atakaye watakaa kwa moto watu waliojiweka tayari. Yeye peke yake atawabatiza katika ROHO MTAKATIFU.  Ubatizo wa Yohane waliendelea kuutumia Wafuasi wa KRISTO "Yohana 4: 1-2 Kwahiyo Bwana alipofahamu ya kuwa Mafarisayo wamesikia ya kwamba Yesu anafanya wanafunzi wengi kuliko Yohane,  na kuwabatiza 2.lakini Yesu mwenyewe hakubatiza,  bali wanafunzi wake."
    Ubatizo huo utatumika mpaka utakapotanguliwa na Yesu kwa kuwekwa namna mpya ya ubatizo. (Matendo 1: 5 "ya kwamba Yohane alibatiza kwa maji,  bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache." Rumi 6:4 "Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake,  kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba,  vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima" )
  YESU ANABATIZWA, Ingawa Yesu hakuwa na dhambi "Yohana 8: 46 Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli mbona hanni sadiki? "
  YESU alikubali kubatizwa na YOHANE kwani hiyo ndiyo hatua aliyotaka MUNGU "Luka 7: 29-30 Na watu wote na watoza ushuru waliposikia hayo,  walikiri haki ya Mungu,  kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohane. Lakini,  Mafarisayo na Wanasheria  walilipinga shauri la Mungu juu yao,  kwakuwa hawakubatizwa naye. "
  Kubatizwa kwa Yesu ilikuwa ni matayarisho ya mwisho kwaajili ya nyakati za Kimasiya. Kwa kitendo hicho Yesu alitaka kuridhisha haki ya Mungu awezayo kuidai ili sisi tupate wokovu "mathayo 3: 15 Yesu akajibu akamwambia "kubali hivi sasa, kwakuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akakubali. " 
        Katika kitendo hicho cha ubatizo,  Mwinjili Mathayo afikiri pia haki mpya  ya Yesu ambayo kwayo ataitimiliza na kuikamilisha haki ya Agano la Kale "Mathayo 5: 17-20 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua Torati au Manabii; la,  sikuja kutangua bali kutimiliza. 18.kwa maana Amin,  nawaambia,  mpaka mbingu na nchi zitakapoondolewa, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka hata yote yatimie.  19.Basi mtu yeyote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni.  Bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha,  huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.  20.Maana nawaambia haki yenu isipozidi hiyo haki ya Waandishi na Mafarisayo,  hamtaingia kamwe katika Ufalme wa Mbinguni.
      UBATIZO WA KIKRISTO. Huu ni ubatizo katika Roho Mtakatifu kama ilivyotangazwa na Yohane Mbatizaji(mt 3: 11 ) . Pia Yesu anaahidi ubatizo huo utaanza na kumiminwa kwa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste "matendo 2: 1-4 Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwapo wote mahali pamoja. Kukaja ghafla toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi,  ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana,  kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine,  kama Roho alivyowajalia kutamka. "
    Halafu Mitume wataendelea kutoa ubatizo na maji "matendo2: 41 ~Nao waliolipokea Neno lake Wakabatizwa,  na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.  8: 12,38~Lakini walipomwamini Filipo,  akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu,  na jina lake Yesu Kristo wakabatizwa wanaume na wanawake,  38~Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini,  Filipo na yule Towashi; naye akambatiza.  Rejea pia matendo 9: 18, 10: 48, 16: 15,33
      Kadiri ya maagizo ya KRISTO(MT 28: 19) ni kama unyago wa kumwingiza mtu katika Ufalme wa Masiya,  lakini watatoa ubatizo huo katika Jina la Yesu "mdo 2: 38~Petro akawaambia " Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu,  nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. "
       Tena ubatizo huo utatolewa kwa yule mwenye kusadiki  katika matendo ya wokovu ya Yesu, "Rumi6: 4~Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake,  kusudi la Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.
     Ubatizo na Imani Huandamana pamoja, "Galatia 3: 26-27~Kwakuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya Imani katika Kristo Yesu.  Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. "Efeso 4: 5~Bwana mmoja, Imani moja,  Ubatizo mmoja." "Ebrania 10: 22~na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani,  hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya,  tume ishwa miili kwa maji safi. "
          Mapato ya ubatizo huu ni yale yale "Galatia 2: 16-20~hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria bali kwa imani ya Kristo Yesu, sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakaye hesabiwa haki.  Lakini ikiwa Sisi wenyewe kwa kutafuta kuhesabiwa haki katika Kristo,  tulionekana kuwa wenye dhambi,  je, Kristo amekuwa mtumishi wa dhambi?  Hasha!  Maana nikiyajenga tena yale niliyoyabomoa,  naonyesha ya kuwa mimi mwenyewe ni mkosaji.  Maana mimi kwa njia ya sheria naliifia sheria ili nimwishie Mungu. Nimesulibiwa pamoja na Kristo,  lakini ni hai,  wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu,  na uhai nilio nao sasa katika mwili,  ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda akajitoa nafsi yake kwaajili yangu. Rejea pia Rumi 6: 3-9
       Ubatizo wa Kikristo una nguvu ya kuondolea dhambi na kumpa mtu Roho Mtakatifu (mdo 2:38)
Watu wa zamani hubatizwa kwa kutosha majini,  na maana ya neno ubatizo kwa Wagiriki ni kutoka majini.  Tendo hili la kutosha na kutoka majini latumika na Paulo kama mfano "Rumi 6: 3-7~Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu,  tulibatizwa katika mauti yake.  Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama tulivyounganika naye katika mfano wa mauti yake,  kadhalika tutaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake. Tukijua neno hili ya kuwa utu wetu wa kale Ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tuitumikie dhambi tena. Kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi.
      Kutoswa majini maana yake mkosefu azikwa pamoja na Kristo "Kolosai 2: 12~mkazikwa pamoja naye katika ubatizo,  na katika huo mkafufuliwa pamoja naye,  kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu"
        Kutoka majini maana yake mkosefu afufuka na Kristo "Rumi 8: 11~Lakini ikiwa Roho wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa,  kwa Roho wake anayekaa ndani yenu" ili awe kiumbe kipya au mtu mpya "2kor5: 7, Efeso 2: 15" au viungo vya mwili mmoja vihuishwavyo na Roho mmoja "1kor 12: 13"
         Ufufuko huo utakuja kukamilika mwisho wa dunia "1kor15: 12~Basi,  ikiwa Kristo anahubiriwa yakwamba amefufuka katika wafu,  mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna ufufuo wa wafu?
         MAANA YA UBATIZO KADIRI YA
                            BIBLIA
Ubatizo kadiri ya Biblia  unaelezwa kwa habari nyingine zaidi ya huko kufa na kufufuka katika Kristo.
         Maana za ubatizo Kibiblia ni: -
  Kumtakasa mtu (Efeso 5: 26>ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika Neno,  Ebrania 10: 22>Na tukaribie wenye moyo wa kweli kwa utimilifu wa imani,  hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya,  tumeshaona miili kwa maji safi)
     Pengine ni kuzaliwa kupya(Yohana 3: 5>Yesu akajibu, "Amin, Amin, nakuambia; Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho,  hawezi kuuingia ufalme wa Mungu,  Tito 3: 5>si kwasababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi, bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa,  kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu. )
      Pengine ni kuangazwa kupya(Ebrania 6: 4>Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru na kulionja kipawa cha Mbinguni na kufanywa washiriki wa Roho Mtakatifu, 10: 32>Lakini zikumbukeni siku za kwanza ambazo mlipokwisha kutiwa nuru, mlistahimili mashindano makubwa ya maumivu)
      Kadiri ya 1Petro 3: 21, safina ya Nuhu ni mfano wa ubatizo. (Mfano wa mambo hayo ni ubatizo unaowaokoa ninyi pia siku hizi,  siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili,  bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.
       Ubatizo mfano wa mateso ya Kristo(Marko 10: 38>Yesu akawaambia, "hamjui mnaloomba. Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi,  au kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi?,  Marko 14: 36>Akasema, " Aba,  Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; walakini si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe)

     
    NB:       sijaona mahali katika Biblia ubatizo ulifanyika mahali pengine tofauti na mto Yordani.
                    Kisha nikajiuliza kwanini waamini wa leo hatuendi kubatizwa mto Yordani?

JIBU NILILOPATA: ni taratibu zilizowekwa na washirika ili kufanikisha kwa urahisi na kwa watu wote agizo la BWANA YESU.
               Nikajiuliza tena wamewezaje kuweka taratibu hizo?  wamepata wapi kibali?

JIBU NILILOLIPATA:  ni mathayo 18: 19-20>>Tena nawaambia ya kwamba,  wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliomba,  watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwakuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu,  nami nipo katikati yao.

          Hapo nikaishiwa maswali.

                            Je,
                 wewe una maswali?





                 BARIKIWA SANA.

NI MIMI,
            MFUASI NA MWANAFUNZI
                    WA YESU KRISTO
    
                 BADIANI Z. KINWIKO.
               
             



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni